BETI NASI UTAJIRIKE

KABWILI ASHINDWE YEYE TU ILA KOCHA MPYA WA YANGA AMEMWELEWA

Mlinda lango kinda Ramadhani Kabwili ni miongoni mwa wachezaji waliomvutia kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael baada ya kumshuhudia 'mbashara' kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar


Eymael alieleza kuvutiwa na uwezo alioonyesha Kabwili licha ya umri wake kuwa mdogo
Huenda Eymael  atampa nafasi zaidi ya kucheza licha ya kuzunguukwa na walinda lango bora Farouk Shikhalo na Metacha Mnata

Msimu uliopita Kabwili alijihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza baada ya aliyekuwa mlinda lango namba moja Beno Kakolanya (sasa yuko Simba) kufanya mgomo
Kabwili alipata nafasi mbele ya Klaus Kindoki ambaye kiwango chake kilikuwa hakitabiriki
Katika msimu huo Kabwili alipata nafasi ya kudaka michezo mingi ukiwemo mchezo dhidi ya Simba

Lakini pia mwaka juzi Kabwili aliingia kwenye vitabu vya kumbukumbu Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) akiwa mchezaji mdogo kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa akidaka mchezo dhidi ya Township Rollers wakati huo akiwa na umri wa miaka 17

Post a Comment

0 Comments