BETI NASI UTAJIRIKE

JULIO: YANGA WAMEUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameibuka na kusema kuwa Kocha mpya waliyemsajili Yanga, Luc Eymael, anaweza akaipeleka pabaya timu hiyo badala ya kuipa mafanikio.


Julio ameeleza kuwa Yanga ni kama wamekurupuka kufanya usajili wa Eymael kutokana na timu ilikuwa imeshaanza kurejea kwenye morali kama zamani.

Amefunguka kwa kushangazwa na namna Yanga ambavyo wamefanya haraka kutafuta kocha mwingine badala ya kumuachia Boniface Mkwasa majukumu ya kuendelea na kazi walau mpaka mwisho wa msimu huu.

Julio amesema Yanga ni kama wameuziwa mbuzi kwenye gunia, anaamini Aymael si sahihi ndani ya timu na hilo ameeleza limechagizwa na kupoteza mechi zake mbili za mwanzo, sambamba na kauli ya ubaguzi aliyoisema baada ya kupoteza dhidi ya Azam FC.

"Hawa Yanga naweza kusema ni kama wameuziwa mbuzi kwenye gunia, hauwezi kumleta kocha mwingine wakati timu imeshaanza kuonesha mwanga mzuri.

"Katika kipindi kama hiki walipaswa kumuachia Mkwasa timu aende nayo walau mpaka mwisho mwa msimu huu".

Post a Comment

0 Comments