Manchester United walizomewa na mashabiki wao baada ya Burnley kuweka ushindi wa kwanza katika uwanja wa mechi ya ligi ya Uingereza katika uwanja wa Old Trafford jana Jumatano usiku.
Burnley walichukua uongozi kabla ya kipindi cha kwanza baada ya Chris Wood kufunga akiwa maguu sita.
Jay Rodriguez aliongeza bao la pili na kuwapatia The Clarets fursa wakati aliposhirkikana na Wood katika nipe nikupe kabla ya kupiga kombora kali kutoka kona ya upande wa kushoto lililomwacha kipa Davdi de Gea bila jibu.
Ni msimu wa tatu mfululizo kwa Burnley kuwa mbele 2-0 katika uwanja wa Old Trafford, lakini ni mara ya kwanza ambapo walizuia na kutoka na ushindi wa pointi zote tatu.
United waliokosa huduma za mshambuliaji nyota Marcus Rashford , walikuwa na bahati mbaya katika kipindi kirefu na hakuwakuweza kumtishia kipa wa Burnley Nick Pope.
Walisomewa katika kipindi cha mapumziko na baada ya mechi kukamilika na mashabiki wengi walitoka katika uwanja huo katika kipindi cha dakika tano za mwisho.
Mazungumzo mengi yalikuwa jinsi Man United itakavyocheza bila Rashford ambaye anauguza jeraha kwa kipindi cha wiki sita.
Hiyo ilimpatia fursa Anthony martial kuonyesha umahiri wake kama mshambuliaji wa nyota wa United, akini mshambuliaji huyo alishindwa kufurukuta katika kipindi chote na alikosa nafasi nzuri katika kipindi cha kwanza kupitia pasi za Wan -Bissaka na Nemaja Matic.
Solskjaer alimuingiza kinda mason Greenwood katika kipindi cha kwanza na kijana huyo alionyesha umahiri wake baada ya kumchenga Charlie Taylor na kupiga nje. Hatahivyo hmatokoe hayo ynaweza kuishinikiza United kununua wachezaji wapya katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari.
0 Comments