Mshambuliaji mpya wa Yanga, Benard Morrison ndiye mchezaji gumzo zaidi kuliko wengine wote katika kikosi cha Yanga.Morisson ameifungia Yanga bao lake la kwanza la michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports
wakati ikiivaa Prisons ya Mbeya na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, jana.Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, pamoja na kuibuka na ushindi, Morrrison alikuwa gumzo kwa kufunga bao lakini bado mbwembwe zake za kuukanyanga mpira juu au kutoa pasi za visigino ziliwafanya mashabiki wa Yanga kuchanganyikiwa kwa furaha.
Kutokana na hali hiyo, Morrison amekuwa gumzo kutoka sehemu mbalimbali, wengi wakimzungumzia kutokana na kazi yake hiyo.Baadhi wamekuwa wakipinga kuwa aina ya uchezaji haionyeshi umakini lakini wengi hasa marshabiki wanaomuunga mkono wamekuwa wakisisitiza kuwa anastahili kujiachia kwa kuwa timu yake ilikuwa inaongoza na inahitaji kuwa na mpira muda mwingi.
Morrison aliwahi kukipiga Orlando Pirates ya Afrika Kusini na amekuwa mmoja wa wachezaji gumzo tokea anajiunga Yanga.
0 Comments