BETI NASI UTAJIRIKE

HIZI HAPA SABABU ZILIZOMPA TUZO YA UCHEZAJI BORA MWAKA 2019 SADIO MANE

Mchezaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa Senegal Sadio Mane amebuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2019 akiwamwaga Mohammed Salah na Mahrez.


Nimekuandalia sababu tatu zilizomfanya Sadio Mane kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa Afrika mwaka 2019

1. Mfungaji bora Ligi kuu Uingereza 

Sadio Mane ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwa mmoja kati ya wafungaji bora ligi kuu Uingereza. Sado Mane, Mohammed Salah na Piere Aubemayang wote walitwaa kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao 20 Ligi kuu Uingereza.

2. Makombe ya Ulaya 

Sadio Mane ametwaa makombe matatu makubwa msimu wa 2018/19. Kombe la Ligi ya mabingwa Ulaya ,Kombe la UEFA SUPER CUP na kombe la CLUB WORLD CUP. Makombe hayo ametwaa akiwa na klabu ya Liverpool akishirikia na Mohammed Salah.

3. Kombe la mataifa Africa 

Sadio Mane alikuwa ni msaada mkubwa kwa timu yake ya Taifa kwenye kombe la mataifa ya Africa yaliyofanyika nchini Misri na kufanikiwa kufika fainali waliyopoteza dhidi ya Algeria  kwa bao 1-0.

Kwa sifa hizo Sadio Mane anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika akiwamwaga Mohammed Salah wa Liverpool na Mahrez wa Manchester City. Sherehe ya utolewaji wa tuzo hizo ulifanyika jijini Cairo nchini Misri na Mtanzania Diamond Platinumz alitumbuiza kwenye sherehe hizo.

Post a Comment

0 Comments