BETI NASI UTAJIRIKE

HIZI HAPA REKODI 3 ALIZOWEKA MORRISON NDANI YA YANGA

Bernard Morrison amewataka wapenzi na mashabiki wa Yanga kumvumilia kwani hapo ndipo kwanza anatafuta fitinesi na kwamba akizoeana na wenzake watafurahia shoo
yake.


Morrison amejiunga na Yanga kwenye dirisha dogo lililofungwa Januari 15, mwaka huu akiwa ni miongoni mwa mastaa wapya saba waliosajiliwa kwenye dirisha hilo. Wengine ni Eric Kabamba, Adeyum Saleh, Tariq Seif, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima na Yikpe Gislain.

Morrison alisema mashabiki wa Yanga waendelee kumvumilia zaidi kwani ana matumaini ya kufanya makubwa mara tu atakapozoeana na wenzake.

Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kucheza mechi yangu ya kwanza salama, hivyo niwaahidi mashabiki wetu nitaendelea kufanya vizuri kadiri nitakavyozoeana na wenzangu maana nilikuwa nje ya uwanja kwa muda, nikipata mazoezi zaidi nitawafurahisha kila mechi.

“Kikubwa naomba ushirikiano kwa wachezaji wenzangu na benchi la ufundi kwa jumla kwani hakuna ushindi bila ushirikiano, kukiwa na ushirikiano siwezi kushindwa kuifanikishia ushindi timu yangu muda wote ninapopangwa,” alisema Morrison.

Morrison avunja rekodi tatu Yanga Akitoa mchango mkubwa katika ushindi wa kwanza tangu mwaka 2020 uingie, mshambuliaji huyo ameweka rekodi tatu akivaa jezi ya Yanga kwa mara ya kwanza akiichezea timu hiyo.

Morrison mwenye uwezo wa kukokota mpira huku akipiga chenga, alitua Yanga akitokea Motema Pembe ya DR Congo baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita. Kabla ya hapo, aliichezea Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Kiungo huyo juzi alicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga huku akifanikiwa kuonyesha kiwango kikubwa katika mchezo huo ambao alihusika kwenye mabao mawili huku akimtengenezea asisti Mnyarwanda Haruna Niyonzima.

Rekodi yake ya kwanza kuiweka akiwa na timu hiyo ni kuipa ushindi Yanga kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida ambao tangu ilipopanda daraja misimu mitatu iliyopita Yanga haikuwahi kupata ushindi katika uwanja huo zaidi ya kuambulia sare na vipigo.

Rekodi ya pili aliyoiweka katika mchezo huo, ni kucheza mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo huku akihusika katika mabao yote matatu kati ya hayo ni la David Molinga alilolifunga dakika 11 ambalo yeye alimpigia pasi ya kichwa Mapinduzi Balama kabla ya kumpasia Molinga na kufunga.

Bao la pili alilolifunga Niyonzima, yeye alipiga krosi safi kwa kiungo huyo fundi baada ya kumtoka beki wa pembeni wa Singida United, Aaron Lulambo kwa kumpiga chenga ya kibaiskeli kabla ya kupiga krosi na mpira kumkuta Niyonzima na kupiga shuti kali ndani ya 18.

Morrison alihusika katika bao la tatu baada ya kupiga kona safi iliyotokana na yeye ambayo iliokolewa na mabeki wa Singida kabla ya Papy Tshishimbi kupiga shuti lililookolewa. 

Post a Comment

0 Comments