BETI NASI UTAJIRIKE

HIVI NDIVYO MWANAUME KAMILI ALIVYOTANGAZWA KUSAJILIWA NA ASTONVILLA

Aston Villa wametangaza rasmi kumsajili nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta akitokea KRC Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne na nusu.Samatta yupo Villa Park hadi (2024) 
kocha wa Aston Villa Dean Smith mapema leo akiongea na waandishi wa habari alisisitiza kuwa mchezaji huyo kila kitu kimekamilika bado vitu vidogo tu.
Hata hivyo Samatta ,27, hatoweza kucheza mchezo wa kesho wa Aston Villa dhidi ya Watford kwa kuwa hakupata muda wa kutosha kuwa na timu hiyo kutokana na kuchelewa kupata kibali cha kazi.
Kupitia akaunti za mitandao ya kijamii ya Aston Villa walichapisha habari hiyo huku wakiandika 
"Tunatangaza rasmi kumsajili @samagoal77 kwa mkataba wa miaka minne na nusu #karibusana Post a Comment

0 Comments