BETI NASI UTAJIRIKE

HIVI NDIVYO AZAM FC WALIVYOTUMA SALAMU KWA YANGA

Azam FC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa jana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.


Ushindi huo unaifanya Azam FC inayomikiliwa na Bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake ifikishe pointi 29 katika mchezo wa 14 na kupanda hadi nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 35 za mechi 14 na Coastal Union pointi 30 za mechi 17.


Lipuli FC baada ya kupoteza mchezo wa jana , inabaki na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 17 na sasa ni ya saba.Katika mchezo wa jana uliochezeshwa na refa Athumani Lazi wa Morogoro aliyesaidiwa na Khalfan Sika  na Kassim Safisha wote wa Pwani, mabao ya Azam FC yamefungwa na Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 70.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razack Abalora, Nicolas Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohamed, Oscar Maasai, Bryson Raphael, Joseph Mahundi, Masoud Abdallah ‘Cabaye’, Shaaban Iddi Chilunda/Andrew Simchimba dk79, Obrey Chirwa/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk60 na Iddi Suleiman ‘Nado’. 

Lipuli FC; Agathony Anthony, David Kameta, Paul Ngalema, David Majinge, Novaty Lufunga, Freddy Tangalu, Paul Luyungu/Seif Rashid dk56, Ally Liungo, Edibert Kisatya/Shaaban Ada dk75, Kenneth Masumbuko na Dullah Mwakasala.

Yanga na Azam watacheza mchezo wa kwanza ligi kuu Tanzania bara siku ya Jumamosi 19 mwezi huu katika dimba la taifa . Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kwani vilabu hivyo vinawania ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara

Post a Comment

0 Comments