BETI NASI UTAJIRIKE

KAMA HESABU ZA SVEN ZIKIKUBALI NDANI YA SIMBA BASI MSIPELEKE TIMU ZENU UWANJANI

Hii Simba mnayoiona kali ikiongoza Ligi Kuu kwa tofauti ya pointi sita kileleni kumbe bado sana na ina mashimo kibao ya kujaza, kwa mujibu kocha wa kikkosi hicho, Sven Vandenbroeck.


Mbelgiji huyo aliyethiri kiti cha Mbelgiji mwenzake, Patrick Aussems aliyetimuliwa licha ya kuiongoza kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, amesema ili Simba iweze kushindana kimataifa inahitaji kuongezwa watu kadhaa wa maana kikosini.

Sven amesema ana wachezaji wengi wazuri ukilinganisha na timu nyingine za Ligi Kuu ya Bara, lakini bado sana kushindana na levo za kina TP Mazembe.

“Tukifanikiwa kupata nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao kwa maana Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho Afrika hapo ndio kuna haja ya kuangalia wachezaji wengine tofauti na hawa ambao ninao kwenye timu.
“Ukiwa na timu nzuri kwenye mashindano ya ndani na ili kuthibisha hilo tunatakiwa kuchukua mataji jambo ambalo kwa upande wetu si baya kwani mpaka sasa tuna kikombe kimoja (Ngao ya Jamii), lakini tunaongoza msimamo wa ligi jambo ambalo naamini litakuwa hivyo mpaka mwisho.
“Bado mapema kueleza kama tutachukua ubingwa wa ligi lakini hilo linawezekana kulingana na kikosi changu kilivyo bora na hayo ndio malengo yetu makubwa ambayo yatatupa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Kufanya vizuri Afrika haitakuwa kazi rahisi kutokana ushindani uliopo kule.
“Hakuna siri ya kufanya vizuri zaidi ya kufanya maandalizi ya kutosha, kila mchezaji kujituma kulingana na nafasi yake ambayo anacheza, jambo hilo ndio linachangia pia kutoa nafasi ya kucheza kwa kila mchezaji ambaye yupo ndani ya timu,” alisema.
“Matumaini yangu kadri muda ambavyo unazidi kwenda tutathibitisha kuwa tuna timu nzuri na bora na tunataka kuwa na muendelezo mzuri wa matokeo mfululizo tukicheza katika uwanja wa nyumbani au ugenini kama ambavyo tulivyofanya CCM Kirumba Mwanza,” alisema Sven.

Alipendekeza Kichuya, Luis wasajiliwe
Sven amefafanua pia usajili wa nyota woa wawili waliosajiliwa wakati wa dirisha dogo, Jose Luis Miquissone kutokea UD Songo na Shiza Kichuya aliyekuwa anacheza nchini Misri kuwa aliwahitaji kwenye kikosi chake ndiyo maana aliwaambia mabosi wake wawasajili.
Alisema katika falsafa zake za kufundisha anapenda kuwa na wachezaji wenye asili ya kucheza winga moja kwa moja na wasipungue watano na wote watatumika kulingana na wapinzani wanaokutana nao hasa kuangalia namna gani wanacheza hasa eneo lao la ulinzi.
Luis nimemuona vya kutosha kwani nimekuwa naye katika timu na akimaliza masuala yake ya vibali ataanza kutumika moja kwa moja katika timu na pia Kichuya nitaanza kumuangalia zaidi kwenye mazoezi ambayo tutaanza leo (jana Jumatano) kwa siku tunafanya mara mbili.

“Nikiwa na mawinga asilia kama hawa wenye uwezo mkubwa wa kukimbia kupitia pembeni hilo ndio nalitaka kwani mbinu zangu napenda kushambulia zaidi kwa haraka kupitia pembeni jambo ambalo linahitaji kuwa na wachezaji wa aina hiyo,” alisema kocha huyo Mbelgiji.

Post a Comment

0 Comments