Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ameteuliwa kuwa Mshauri Mkuu Bodi ya Wakurgenzi ya Simba. Makonda anaungana na jopo la wazee kama Magori ambao
humshauri mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji namna yakuendesha kwa mafanikio klabuni hapo.
humshauri mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji namna yakuendesha kwa mafanikio klabuni hapo.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mohammed Dewji 'Mo' amemkaribisha Makonda katika majukumu yake hayo mapya
"Nafurahi sana kumkaribisha RC wetu, Mnyama mwenzangu PAUL MAKONDA kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Simba akiwa kama Mshauri Mkuu (Senior Advisor). Karibu kaka. Pamoja tutajenga SIMBA bora zaidi! Hongera kwa uteuzi," amesema Mo
KILICHOSABABISHA MAKONDA AKATEULIWA SIMBA
Mara baada ya klabu ya Simba kufungwa bao 1-0 kwenye fainali za kombe la mapinduzi ,Mkurugenzi bodi ya Simba Mohammed Dewji alitangaza kujivua nafasi hiyo na kubaki kama mwekezaji wa kawaida. baadhi ya mashabiki wakongwe wa klabuni hapo walianza kumsimanga na kumuhoji Dewji kuhusu uhalali wake kwa Simba kama ni Mwekezaji kweli au mchumia tumbo . Kwa upande wa Makonda yeye alikuwa na maoni tofauti na ujumbe wake umemfanya ateuliwe nafasi ya Mshauri mkuu . Makonda aliandika hivi
0 Comments