BETI NASI UTAJIRIKE

HESABU ZA SVEN ZAWATISHA MASHABIKI WA YANGA

Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amefunguka kuwa amejipanga kushinda kila mchezo katika Ligi Kuu Bara ukiwemo dhidi ya Yanga kwa kuwa malengo yake ni kutetea ubingwa wa ligi  kuu Tanzania bara.Mbelgiji huyo mpaka sasa akiwa na Simba amefanikiwa kuiongoza timu hiyo kwenye mechi nne, tatu za Ligi Kuu Bara ambazo amefanikiwa kuchukua pointi tisa na moja ikiwa ni ya Kombe la FA.

Simba inatarajia kucheza na Yanga Januari 4, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Vandenbroeck alisema kuwa licha kupata muda mdogo wa kufanya maandalizi ya timu yake, lakini malengo yake ni kuhakikisha anashinda kila mchezo uliopo mbele yake ukiwemo wa Yanga ili kujihakikishia ubingwa.

Unajua tumecheza mechi tatu katika siku saba, nadhani tunabadilika, tunafanya mazoezi mara moja ila mechi hazina idadi lakini hatuwezi kutoka nje ya malengo yetu.

“Kiukweli hakuna jambo rahisi kwetu lazima tupambane ili kufikia malengo kutokana na ubora wa timu yetu, hatuwezi kuangalia nani anakuja mbele zaidi ya kujikita kwenye malengo ya kushinda pointi tatu, Yanga ni wazuri lakini kwetu tunachoangalia ni kuchukua pointi tatu kwao ili kufikia malengo,” alisema Vandenbroeck.

Post a Comment

0 Comments