bao pekee la mshambulaji Ayoub Lyanga dakika ya 77 limetosha kuipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Kwa ushindi huo, Coastal Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 16 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 35 za mechi 14, wakati Azam FC sasa ni ya tatu kwa pointi zake 26 za mechi 13.
JKT Tanzania wamepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, bao pekee la Edson Katanga. Nayo Namungo FC ikapata ushindi wa ugenini wa 3-2 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
0 Comments