BETI NASI UTAJIRIKE

GOLIKIPA SHIKHALO AWATUMIA UJUMBE WANAYANGA KUELEKEA MCHEZO WA BAADAYE

Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo amesema pamoja na kikosi chao kutokuwa na mwenendo mzuri, watarejea kwenye ubora wao tena wakiwa imara.Yanga imecheza mechi tatu mfululizo za ligi kuu bila ya kupata ushindi


 ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Simba kabla ya kupoteza michezo dhidi ya Kagera Sugar na Azam Fc.Mlinda lango huyo wa Kimataifa wa Kenya amesema wakati mwingine ni lazima kupitia nyakati ngumu ili kutengeneza njia ya mafanikio

"Tumeshushwa chini na tunapita kwenye wakati mgumu, lakini amini kila changamoto inakuwa na njia ya mafanikio, tutarejea tukiwa imara," ameandika Shikhalo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Kesho Yanga itashuka kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida kuwakabili wenyeji wao Singida United katika mchezo ambao mabingwa hao wa kihistoria wanahitaji ushindi

Post a Comment

0 Comments