BETI NASI UTAJIRIKE

DIAMOND AMCHEZESHA TETEMA RAIS WA FIFA , SADIO MANE ATOA NENO

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na C.E.O wa Wasafi Media Diamond Platnumz alipata nafasi ya Kuperform katika tukio la utoaji tuzo lililofanyika katika taifa la Misri.

Katika tuzo hizo mchezaji wa taifa la Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane alifanikiwa kushinda tuzo hiyo akiwashinda wachezaji Mohamed Salah anayejipiga katika klabu ya Liverpool pia na timu ya taifa ya Misri na Riyad Mahrez anayejipiga katika katika klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Algeria ingawa Maherz alishinda tuzo ya goli bora la michuano ya AFCON.
Katika tukio hilo msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz alipata nafasi ya kutumbuiza katika tukio hilo na kuweza kuwaburudisha wageni wote waliofika katika tukio hilo ambapo wachezaji wa zamani kama Samuel Etoo nata Sadio Mane na rais wa FIFA Gianni Infantino alionyesha kufurahishwa na show hiyo ya Diamond Platnumz.

Baadaya kushinda tuzo hiyo Sadio Mane aliongea maneno haya:-Aliweza kufunga magoli 15 mpaka sasa kwa mwaka 2019 mpaka 2020, na kuisaidia Liverpool kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 13.
“Nina furaha sana na ninajivunia kuwa mshindi. Kandanda ni ajira yangu ambayo ninaipenda,” alisema Mane.
“Ninapenda kuwashukuru familia yangu, taifa langu , timu yangu ya taifa , wachezaji wenzangu, shirikisho na klabu ya Liverpool.Hii ni siku kubwa kwangu.”
Mane alichukua tuzo yake katika sherehe zilizofanyika huko Hurghada, Misri.
Lakini si Salah, ambaye alishinda tuzo hiyo mara mbili katika miaka miwili iliyopita wala Mahrez wali.
Sadio ManeHaki miliki Sadio Mane ameifungia Liverpool magoli 15 kwa mwaka 2019-20
Mane alimaliza katika nafasi tatu za juu katika tuzo hizo katika miaka mitatu iliyopita.
Na ilikuwa ni ndoto yake kushinda tuzo hiyo ili kufikia mafanikio ya shujaa wake El Hadji Diouf, ambaye alishinda mwaka 2002.
Mahrez alishinda tuzo moja – Goli bora la Afrika ambalo alilifunga kwenye mchezo wa nusu fainali Afcon kati ya Algeria na Nigeria .
Salah, Mane na Mahrez wote wameingia katika kikosi cha wachezaji 11 bora pamoja na beki wa kati wa Liverpool, Joel Matip na beki wa kulia wa Tottenham Serge Aurier na mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang.
Wachezaji bora 11 wa Afrika: Andre Onana (Ajax/Cameroon), Achraf Hakimi (Borussia Dortmund/Morocco), Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal), Joel Matip (Liverpool/Cameroon), Serge Aurier (Tottenham/Ivory Coast), Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria), Idrissa Gana Gueye (Paris St-Germain/Senegal), Hakim Ziyech (Ajax/Morocco), Mohamed Salah (Liverpool/Egypt), Sadio Mane (Liverpool/Senegal), Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/Gabon)
Beki wa kulia wa Morocco,Achraf Hakimi mwenye miaka 21,ambaye anachezea Borussia Dortmund kwa mkopo akitokea Real Madrid, ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
Mshambuliaji wa Nigeria na Barcelona Asisat Oshoala ametajwa kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake akiwapiku mshambuliaji wa Cameroon Ajara Nchout na nyota wa Beijing BG Phoenix na Afrika Kusini Thembi Kgatlana.
Cameroon, waliopoteza mbele ya England kwa 3-0 kwenye hatua 16 bora ya fainali za kombe kwa wanawake mwaka 2019 wameshinda tuzo ya kuwa timu bora ya taifa kwa upande wa wanawake.
Djamel Belmadi, aliyeiongoza Algeria kushinda ubingwa wa Afcon ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, na kocha wa Afrika ya kusini Diseree Ellis, akishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Post a Comment

0 Comments