Kama Samatta atasajiliwa na klabu hiyo basi atakuwa ni mchezaji wa kwanza kucheza ligi kuu nchini Uingereza , Msimu huu aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza ligi ya Mabingwa ulaya huku akiwafunga mabingwa watetezi wa michuano hiyo Liverpool.
Dau la Samatta
Inasemekana dau la Samatta ni Paundi milioni 8.5-10 sawa na bilioni 24 mpaka 30 za kitanzania. Fedha hizo ni nyingi mno na kama zitalipwa basi kunauwezekano klabu ya Simba ikanufaika na mgao huo kutokana na mkataba kati ya Simba na Mazembe endapo mchezaji huyo atauzwa kwenda klabu yoyote.
Taarifa zinasema Simba ilinufaika na gawio kutoka TP Mazembe baada ya klabu hiyo kumuuza kutoka TP Mazembe kwenda KRC Genk ya nchini Ubelgiji. Bado taarifa rasmi haijawekwa wazi kama Simba watanufaika na gawio hilo.
Matumizi ya dau la Samatta
1. Ununuzi wa magari
Dau la Samatta linatosha kumnunulia kila mchezaji anayecheza ligi kuu Tanzania bara magari matatu aina ya IST. jumla ya wachezaji wanaocheza ligi kuu ni 600 hivyo dau la samata linatosha kununua magali 2,250 na wachezaji hao kupata magari matatu kila mmoja yenye thamani ya milioni 12.
2. Ujenzi wa Viwanja
Dau la bilioni 30 za kitanzania linatosha kujenga viwanja 10 vikubwa kama kile cha Azam Complex kinachomilikiwa na klabu ya Azam FC pale Chamanzi chenye thamani ya bilioni 3
UWANJA WA AZAM COMPLEX THAMANI YAKE NI BILIONI 3
Kama dau hilo litatumika kujenga viwanja vya mazoezi kama kile cha Simba pale bunju basi viwanja 40 vitajengwa kwa dau hilo.
Uwanja wa Simba thamani yake ni milioni 500
0 Comments