BETI NASI UTAJIRIKE

TFF WATOA TAARIFA KUHUSU KOCHA WA YANGA KUBAGULIWA MECHI NA AZAM

Kamati ya Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) imetoa onyo kali kwa Kocha wa Yanga Luc Eymael kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa kuhusu ubaguzi wa rangi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara


dhidi ya Azam FC uliochezwa Januari 18, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Stephen Mguto amesema kamati hiyo pia imeiomba Yanga kutoa tamko juu ya kauli hizo pamoja na vitendo vingine alivyoeleza kuwa siyo vya kiungwana.

Kuhusu malalamiko ya kocha huyo kuwa alibaguliwa, Mguto amesema alichofanyiwa na mwamuzi Hans Mabena hakikuwa ubaguzi wa rangi.

Sisi hatukuliona kama ni ubaguzi ..Maneno yake aliyosema kwamba amebaguliwa kwa sababu yeye ni mweupe, hayana maana”, amsema Mguto.

Post a Comment

0 Comments