BETI NASI UTAJIRIKE

UONGOZI YANGA WAZUNGUMZIA KIPIGO CHA AZAM FC

Uongozi wa klabu ya Yanga umewaomba radhi wapenzi, wanachama na mashabiki wake baada ya kupoteza mchezo wa pili mfululizo kwa kufungwa bao 1-0 na Azam Fc


Afisa Mhamasishaji wa timu hiyo Antonio Nugaz amesema, benchi la ufundi linaendelea kupambana kuirejesha timu kwenye ubora wake

"Tunawaomba radhi mashabiki na wanachama wetu baada ya kupoteza mchezo leo, mapambano bado yanaendelea tuendelee kushikamana naamini furaha itarejea kwa kishindo," amesema

Baada ya mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jana, mashabiki walionyesha hasira zao kwa kuutupia lawama uongozi kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya
Mashabiki wengi wanaamini mabadilko ya benchi la ufundi ndio chanzo kwa timu kupoteza mwelekeo

Post a Comment

0 Comments