BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAMTAJA ANAEIHUJUMU TIMU NA KUSABABISHA IFUNGWE MECHI 3 MFULULIZO

Mwezi huu Yanga imemleta kocha mpya Luc Eymael kuwa mrithi wa Mwinyi Zahera aliyetimuliwa mwezi Novemba 2019. Lakini kabla ya ujio wa kocha mpya, Yanga ilikuwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu Charles Mkwasa


Kumekuwa na mjadala juu ya nini kinaisibu Yanga sasa kwani tangu Eymael awasili timu imefungwa mechi zote.wapo wanaodhani kuna jambo haliko sawa kwenye benchi la ufundi
Baadhi wametoa maoni kuwa ni vyema uongozi wa Yanga ukamuondoa Mkwasa kwenye benchi la ufundi ili kuwaacha makocha wapya wawe huru kutimiza majukumu yao.

Kocha Kenny Mwaisabula ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, amesema Mkwasa tayari amemaliza majukumu yake hivyo hapaswi kuendelea kuwa kwenye benchi la ufundi

Lakini pia wapo wanaoamini Mkwasa anastahili kuendelea kuwepo ili kuwasaidia makocha wapya kwani bado hawawafahamu wachezaji
Je mdau ni yepi maoni yako, Mkwasa aondolewe kwenye benchi la ufundi au abakishwe?

Post a Comment

0 Comments