Kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya yuko tayari kuanza majukumu kunako mabingwa hao wa nchi baada ya kupata leseni.Kichuya alirejeshwa Simba usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Pharco Fc ya Misri
Tayari ameanza mazoezi na kikosi cha Simba, timu aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa kwa misimu mitatu kabla ya kuuzwa mwaka jana
Huenda akaanza rasmi kuonekana dimbani kwenye mchezo wa kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Jumamosi, Januari 25 kwenye uwanja wa Uhuru
Pacha wake waliyetua nae dirisha dogo Luis Miquissone naye alikuwa akisubiri kuwasili kwa hati yake ya uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili aanze kuichezea Simba kwenye mechi za kimashindano
Miquissone alipata nafasi ya kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi
0 Comments