Kwa mara nyingine leo Yanga imeonyesha kuendelea kuimarika ikipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida United katika mchezo uliopigwa uwanja wa LITI Singida.Ilikuwa mara ya kwanza kwa Yanga
kupata ushindi kwenye uwanja huo ambao zamani ulikuwa ukiitwa Namfua
kupata ushindi kwenye uwanja huo ambao zamani ulikuwa ukiitwa Namfua
Lakini jambo la kuvutia zaidi ni ubora ulioonyeshwa na kikosi cha Yanga kinachonolewa na kocha Luc Eymael
Kwa mchezo wa pili mfululizo Yanga inatawala, huku leo safu ya ushambuliaji ikionekana kuongeza umakini na kufanikiwa kufunga mabao matatu
Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ameongeza ubunifu kwenye safu ya ushambuliaji Yanga
Leo Yanga ilimiliki mpira wa asilimia 60, muda mwingi Singida United walikuwa wakiusaka mpira kwa tochi
Walivyocheza Yanga leo sio tofauti sana na mchezo waliocheza dhidi ya Azam Fc, wamekuwa bora katika umiliki wa mpira kwenye michezo yote miwili
Eymael ni kocha anayependa soka la kuvutia, pasi nyingi na kushambulia kwa kasi
Nadhani falsafa yake imeanza kufanya kazi, hakika kuna mambo ya kufurahisha yanakuja Yanga
0 Comments