BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WATAKA KAMATI YA MASAA 72 KUTOA HUKUMU KWA SULTANI WAWA

Jana Kamati ya Saa 72 ilitoa adhabu mbalimbali kwa timu zinazoshiriki ligi kuu kulingana na makosa mbalimbali yaloyofanyika kwenye ligi tangu kuanza kwa mwaka huu


Wakati Yanga ikionekana kinara wa kuadhibiwa, kuna matukio ya dhahiri ambayo yalijitokeza lakini wengi wanashangaa hatua hazikuchukuliwa  zaidi ni tukio la beki wa Simba Paschal Wawa kumkanyaga kwa makusudi mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa Januari 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa

Pamoja na kuwa mwamuzi hakuliona tukio hilo, kamera za Azam Tv zililinasa na hata Mwenyekiti wa Bodi ya ligi aliahidi kuwa hatua zitachukuliwa

Lakini katika matukio yaliyotolewa adhabu jana tukio la Wawa halikuwa miongoni
Wakati mwingine matukio kama haya ndio yanayowapa sababu watu kuamini kuwa TFF na Bodi ya Ligi zinafanya kazi kwa kuipendelea klabu ya Simba

Kwani wakati mashabiki wa Yanga wakilalamikia tukio la Wawa, mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere alimpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa uhuru mwaka jana.Lakini pamoja na tukio hilo kupigiwa kelele hakuna hatua zozote zilizochukuliwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto jana alisema baadhi ya matukio bado yanachunguzwa

Wadau hawatachoka kusubiri kuona kama hatua zinachukuliwa ili kuondoa hii dhana ya kuwa kuna upendeleo unafanywa kwa baadhi ya timu

Post a Comment

0 Comments