BETI NASI UTAJIRIKE

UCHAMBUZI : MDAU ACHAMBUA TUKIO LA LUC EYMAEL NA REFA MCHEZO WA AZAM VS YANGA

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael juzi baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc alilalamilkia kitendo cha mwamuzi Hans Mabena kukataa kupokea mkono wake baada ya mchezo na kukifananisha kitendo hicho sawa na ubaguzi wa rangi


Siku moja baadae TFF ikatoa tamko ambalo kimsingi linaonesha kutofurahishwa na matamshi ya Eymael na kuiagiza Bodi ya ligi imchukulie hatua
Lakini kimsingi sioni kosa la Eymael kwani yeye alikuwa ni mhanga wa tukio ambalo pengine hakuwahi kukutana nalo kabla

Eymael amefanya kazi nchi nyingi kabla ya kuja hapa Tanzania hivyo pengine tukio hilo la mwamuzi kugomea salamu yake ni la kwanza kwake

Matamshi aliyotoa ni dhana aliyoijenga kuwa inawezekana alibaguliwa kwani mwamuzi alipokea salamu za wengine wote isipokuwa yeye

Na ieleweke kwa mujibu wa maelezo yake, tukio hilo lilitokea baada ya mchezo na sio wakati alipopewa kadi ya njano na mwamuzi

Lakini pia kocha ana haki ya kulalamika pale anapoona yeye mwenyewe au timu yake haitendewi haki

Eymael alikubali uamuzi uliochukilwa na Mabena kumpa kadi nyekundu Mtoni baada ya kumkanyaga Wadada lakini rafu mbaya aliyocheza Wadada alistahili kupewa kadi tena nyekundu maana alidhamiria kumuumiza Mtoni

Kama angempata Mtoni pengine angeweza kumvunja mguu.Hapa ndipo msingi wa malalamiko ya Eymael ulipoBahati mbaya baada ya kulalamika Mabena akampa kadi ya njano na hata baada ya mchezo akagoma kumpa mkono

Post a Comment

0 Comments