BETI NASI UTAJIRIKE

NGASA AFUNGUKA YALIYOTOKEA MWEZI JANUARI

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa amesema ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Singida United jana umewapa nguvu mpya.Ngasa amesema wachezaji hawakuwa na furaha wakiwa hawajashinda 


mchezo wowote kwenye ligi tangu kuingia kwa mwaka 2020 kabla ya ushindi wa jana
"January ilikuwa ngumu kwetu kupata ushindi Ilikuwa yanichanganya imefanya mpaka nimefungiwa," ameandika Ngasa kwenye mtandao wa Instagram

"Leo tumeshinda, asante mashabiki kwakutupa moyo na kutuamini na leo tumepata matokeo mazuri

"Hongera kwa wachezaji wote kwa kupigania ushindi na hongera wadhamini wetu wote na kubwa GSM"

"Tunawashukuru mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi ya leo,  tunawashukuru sana kuwa nasi katika kipindi cha furaha na huzuni tukiwa pamoja"

Post a Comment

0 Comments