BETI NASI UTAJIRIKE

KWA SIMBA HII YA SVEN NA MATOLA MTASUBIRI SANA WAPINZANI

Simba imerejesha vipigo vya 4G ligi kuu baada ya kuifumua Alliance Fc mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba.Pamoja na kutangulia kufunga bao la kuongoza


 Alliance Fc ilishindwa kwenda na kasi ya mabingwa hao wa nchi waliokuwa na kila sababu ya kushinda mchezo huo kutokana na kuwa bora kuliko wapinzani wao.kiungo Jonas Mkude aliisawazishia Simba bao dakika chache kabla ya kwenda mapumziko Alliance wakitangulia kufunga kupitia mpira wa adhabu kwenye dakika ya 27

Meddie Kagere, Clatous Chama na Hassan Dilunga waliongeza mabao mengine matatu kwenye kipindi cha pili kuihakikishia Simba ushindi mnono

Ushindi huo unazidi kuiweka Simba kileleni mbali zaidi na timu nyingine katika mbio za kuwania ubingwa sasa wanaongoza kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili huku wakiwaacha watani zao Yanga kwa alama 16

Post a Comment

0 Comments