Wakati kina Hassan Dilunga wakiendelea kutupia mabao watakavyo kwenye ligi, kwa wiki kadhaa Simba imemkosa Miraji Athumani mmoja wa wafungaji wake bora sana msimu huu kutokana na majeraha
Habari njema ni kuwa Miraji aliyetupia mabao sita mpaka sasa, amepona majeraha na ataanza mazoezi na timu baada ya mabingwa hao wa nchi kurejea leo kutoka jijini Mwanza
Huenda akawa tayari kuwakabili Mwadui Fc kwenye mchezo wa raundi ya nne kombe la Azam (ASFC) ambao utapigwa Jumamos Januari 25 kwenye uwanja wa Uhuru
Kurejea kwake kutaongeza wigo wa watupia nyavu wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere ambaye amefunga mabao 11
Miraji amefunga mabao sita wakati Hassan Dilunga na Deo Kanda wamefunga mabao manne kila mmoja
0 Comments