Uongozi wa Singida United umethibitisha kumsajili kiungo Raphael Daudi Lothi kutoka klabu ya Yanga kwa mkopo wa miezi sita.Lothi anakuwa mchezaji wa tatu kutua Singida
kwa mkopo akitokea Yanga.Wengine ni walinzi Cleofas Sospeter na Muharami Issa 'Marcelo'.Hata hivyo Lothi hakuwemo kwenye orodha ya awali iliyotolewa na Yanga juzi baada ya dirisha la usajili kufungwa
Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amesema leo watatoa orodha kamili ya wachezaji ambao wataitumikia Yanga na wale ambao wameachwa/kutolewa kwa mkopo
0 Comments