Wakati Yanga ikinolewa na Hans van Pluijm msimu wa 2014/15 na 2015/16, ilikuwa ikicheza kandanda safi la kuvutia.Ni wakati huo wachezaji kama Thabani Kamusoko walisajiliwa na kuasisi aina ya uchezaji uliopachikwa jina maarufu la kampa-kampa tena.
Ni soka la pasi fupi fupi ambalo msingi wake ulitawaliwa na viungo mahiri wakati huo Kamusoko, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke kipindi hicho akiwa wa moto kwelikweli akiwa amejiunga Yanga akitokea klabu ya Mbeya City
Ni soka la pasi fupi fupi ambalo msingi wake ulitawaliwa na viungo mahiri wakati huo Kamusoko, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke kipindi hicho akiwa wa moto kwelikweli akiwa amejiunga Yanga akitokea klabu ya Mbeya City
Lakini baada ya kuondoka Pluijm na kuingia George Lwandamina, chini ya Mzambia huyo Yanga ilibadilika.Lwandamina alitumia zaidi mashambulizi ya kushitukiza pamoja na mipira mirefu
Hata alipokuja Mwinyi Zahera, Yanga haikuwa na mabadiliko ya mbinu za kiuchezaji
alikuwa Charles Mkwasa aliyeanza kurejesha mfumo wa Pluijm katika muda wake mfupi aliokuwa kocha wa muda Yanga
Lakini ujio wa Luc Eymael, umeanza kubadili kabisa aina ya uchezaji wa Yanga
Katika michezo yake miwili iliyopita, sura na mwelekeo wa Yanga yake imeanza kuonekana
Mbelgiji huyo anapendelea soka la kuvutia, pasi nyingi na kuwapa burudani mashabiki
Katika mazoezi ya kikosi chake, Eymael hapendi wachezaji kukaa na mpira muda mrefu, huangalia muda ambao kila mchezaji anakaa na mpira
Ndio maana Yanga yake imeanza kupiga zile pasi moja moja nyingi
Mchezo dhidi ya Azam Fc, pamoja na kufungwa Yanga ilikuwa bora zaidi, na hata jana ilitawala mchezo dhidi ya Singida United
Ni miaka sasa mashabiki hawakuwa wameishuhudia Yanga ile ya kampa-kampatena, hakuna shaka Eymael anairudisha burudani hiyo Jangwani
0 Comments