BETI NASI UTAJIRIKE

ALICHOSEMA KOCHA WA YANGA KUHUSU MORRISON NA USHINDI DHIDI YA SINGIDA

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amepongeza kiwango kilichoonyeshwa na kikosi chake kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida United jana akibainisha kuwa timu inaelekea sehemu sahihi


Eymael alipoteza michezo miwili ya kwanza, lakini kikosi chake jana kimeonekana kuimarika zaidi wachezaji wakicheza kwa kujiamini

"Nimefurahi jinsi wachezaji wangu walivyocheza leo, wameanza kuelewa kile ninachowafundisha mazoezini," amesema
"Walinza kucheza vyema kwenye mchezo uliopita dhidi ya Azam pamoja na kuwa tulipoteza lakini tulikuwa bora"

Amwagia sifa Morisson
Eymar pia alimpongeza kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ambaye jana alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi cha Yanga
Morrison alikuwa chachu ya ushindi wa Yanga akishiriki katika upatikanaji wa mabao yote matatu

"Pamoja na kuwa ni mara ya kwanza anacheza ligi ya Tanzania tena katika uwanja ambao sio mzuri, ameonyesha uwezo mkubwa"

"Ni bahati mbaya nimechelewa kuja hapa, lakini ningeweza kuleta wachezaji wengine wawili ambao wana uwezo kama wake," alisema Eymael

Post a Comment

0 Comments