Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kinaingia kambini kujiandaa na mchezo wa raundi ya nne kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Mwadui Fc
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema timu itaweka kambi ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.Rweyemamu amesema wachezaji wote waliosajiliwa na Simba wataingia kambini kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa Jumamosi Januari 25 katika uwanja wa Uhuru
"Leo timu itaingia kambini Ndege Beach tulipoweka kambi ya kudumu katika msimu huu kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Mwadui," amesema
"Tunafahamu umuhimu mkubwa wa kombe hili, hivyo ni lazima timu yetu ipate matokeo mazuri ili tuendelee na mashindano hayo na mwisho wa siku tuweze kuwa mabingwa"
"Maandalizi yanakwenda vizuri na timu yetu na wachezaji wote wataingia kambini akiwemo kiungo Shiza Kichuya ambaye alikuwa akikamilisha baadhi ya mambo ili aanze kuichezea Simba"
0 Comments