BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA: NI "DO OR DIE" ILA KISASI LAZIMA KILIPWE KWA MWADUI

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo Jumamosi Januari 25 2020 kitashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuikabili Mwadui Fc katika mchezo wa raundi ya nne michuano ya kombe la Azam (ASFC)


Simba ilianza mazoezi juzi kujiandaa na mchezo huo baada ya kurejea kutoka mkoani Mwanza walikoshinda michezo miwili ya ligi dhidi ya Mbao Fc na Allliance Fc

Ni mchezo ambao Simba itakuwa nyumbani, ina kila sababu ya kuibuka na ushindi ili kutinga raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo ni hatua ya 16 bora
Lakini pia huu utakuwa mchezo wa kisasi kwa Simba kwani Mwadui Fc ndio timu pekee liyopata ushindi dhidi ya Simba kwenye ligi

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kinajiandaa kikamilifu ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kutinga hatua inayofuata.Simba inayoendelea kujifua katika uwanja wake wa Mo Simba Arena, itaingia kwenye mchezo huo huku ari ya wachezaji wake ikiwa juu baada ya ushindi wa michezo miwili iliyopigwa jijini Mwanza

Post a Comment

0 Comments