BETI NASI UTAJIRIKE

ZAHERA AWAMWAGIA SIFA MOLINGA NA MORISSON AWAPA JINA LA MO SQUARE

Aliyekuwa Mkufunzi wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu hiyo imeonyesha mabadiliko makubwa ya uchezaji juzi walipoikabili Singida United.Zahera ambaye yupo mbioni kujiunga na Buildcon ya Zambia


Kwa sasa bado yuko nchini akiwa ameweka makazi yake ya muda.Ameeleza kuvutiwa na mbinu za Mbelgiji Luc Eymael ambapo amemtabiria kuwa ataweza kutengeneza timu ya ushindani

"Nimpongeze kocha kwa kuiwezesha Yanga kucheza mpira mzuri na wakuvutia tofauti na mchezo wao uliopita, naamini kama kocha atapewa nafasi ya kufanya kazi yake watakuwa na kikosi bora kwa misimu ijayo," amesema Zahera

"Binafsi sikushangaa matokeo yao ya awali walipofungwa na Kagera Sugar,  nilijua ni ugeni wa mbinu za kocha kwa wachezaji,  lakini kwa sababu wachezaji wengi nawajua nilikuwa na matumaini ya kubadilika kwa kikosi katika mechi zinazokuja, kocha anastahili pongezi hizi"

Aidha Mcongomani huyo amesifu usajili wa kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ambapo amesema mchezaji huyo atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

"Nimemuona mchezaji wao mpya waliomleta juzi (Morrison), ni mchezaji mzuri sana, Nadhani kama kocha ataweza kumtumia vizuri, atawasaidia"
"Mchezaji huyu akitumika vizuri pamoja na Molinga nadhani watafunga mabao mengi"

Zahera alitimuliwa Yanga baada ya timu kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-1 kutoka kwa Pyramids ya Misri
Mcongoani huyo alisajili nyota wapya 12 kwenye kikosi chake, hata hivyo miongoni mwao, nyota watano wa kigeni wameachwa

Wachezaji aliowaleta mwezi Julai lakini tayari wameachwa ni Sadney Urikhob, Juma Balinya, Mustafa Selemani, Maybin Kalengo na Issa Bigirimana

Post a Comment

0 Comments