BETI NASI UTAJIRIKE

MOLINGA , YIKPE WAMHARIBIA ULAJI NCHIMBI

Upo uwezekano mkubwa Yanga itamuuza mshambuliaji wake Ditram Nchimbi kwa klabu moja inayoshiriki ligi kuu ya Misri.Timu hiyo ambayo kwa sasa haitawekwa wazi, iko kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga kukamilisha usajili wake


Dili kama hilo pia litamuhusu kiungo Feisal Salum ambaye nae anaweza kutimkia nchini humo.Lakini nyota hao wametakiwa kwenda kufanya majaribio kabla ya dili zao kukamilishwa.

Uwepo wa Molinga na Yikpe unamfanya Ditram atafute  nafasi ya kucheza kutokana na ubora wa mastraika hao wawili waliouonyesha hivi karibuni. Nchimbi amesajiliwa na Yanga msimu wa dirisha dogo na aligeuka kuwa habari ya mjini baada ya kuifunga timu hiyo mabao matatu akiitumikia polisi Tanzania kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3 .

Tangu kocha Eymael kuwasili klabuni hapo Ditram amekuwa akitokea benchi na mpaka sasa ameshindwa kuonyesha uwezo wa hali ya juu kama ilivyokuwa inategemewa wakati anasajiliwa klabuni hapo

Post a Comment

0 Comments