BETI NASI UTAJIRIKE

KIGOGO YANGA AWAVAA TFF KISA MECHI NA SINGIDA

Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Ruhago ameishukia Bodi ya Ligi kwa kufanya mabadiliko ya ratiba bila kuzihusisha timu husika.Dk Ruhago ametoa malalamiko hayo baada ya Yanga kutakiwa kusafiri kwenda mkoani Singida 


kuikabili Singida United hapo kesho wakati awali ratiba lionyesha mcheoz huo ulipaswa kupigwa mkoani Arusha

"Tayari tulikuwa tumeshaingia gharama ya usafiri pamoja na kambi mkoani Arusha lakini ghafla tunaambiwa tunatakiwa kwenda Singida," amesema Dk Ruhago

Yanga ililazimika kusafiri jana kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida United ambao utapigwa kesho, Jumatano uwanja wa Namfua
Mabingwa hao wa kihistoria walitua Singida jana jioni na leo wanatarajia kufanya mazoezi ya mwisho dimba la Namfua

Post a Comment

0 Comments