BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAITUMIA SALAMU SINGIDA UNITED MCHEZO WA JUMATANO

Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo Yanga inaelekea mkoani Singida kuikabili Singida United katika mchezo unaofuatia wa ligi kuu.Mchezo huo utapigwa Jumatano, Januari 22 kwenye uwanja wa NamfuaKocha Luc Eymael bado anasaka ushindi wake kwa kwanza akiwa na kikosi cha Yanga
Hivyo ni mchezo ambao atahitaji kutumia silaha zake zote kupata alama tatu
Pamoja na uhusiano mzuri kati ya Yanga na Singida United, timu hizo zimekuwa na ushindani mkali dimbani

Singida United imesajili wacheza 17 dirisha dogo, wachezaji watatu Raphael Daudi, Cleofas Sospeter na Muharami Issa 'Marcelo' wamesajiliwa kutoka Yanga
Timu hiyo pia imewaongeza nyota wengine waliowahi kuichezea Yanga Haruna Moshi 'Boban', Haji Mwinyi Mngwali na Athumani Iddi 'Chuji'

Post a Comment

0 Comments