Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amemshukia mwamuzi wa mchezo dhidi ya Azam Fc Hans Mabena baada ya kugoma kumpa mkono baada ya mchezo huo
Eymael amesema tukio hilo ni la kibaguzi
Mbelgiji huyo amesema baada ya Mabema kumtoa Ally Mtoni kwa kadi nyekundu, alilalamikia uamuzi huo kwa kuwa Mtoni alilipa kisasi baada ya kufanyiwa madhambi mwanzo lakini mwamuzi hakuchukua hatua
Amesema baada ya malalamiko yake Mabena alimuonyesha kadi ya njano
Lakini tukio lililomkera zaidi ni kitendo cha mwamuzi huyo kugoma kumpa mkono baada ya mchezo kumalizika
"Tukio hilo naliona kama ubaguzi wa rangi, amefanya hivyo kwa sababu mimi ni mzungu? Mbona wengine aliwapa mkono lakini nilipotaka kumpa mkono wangu aliniambia hawezi kunipa mkono wake," alin'gaka Eymael kwa hasira
0 Comments