BETI NASI UTAJIRIKE

BILIONEA ASHANGAZWA NA UWEPO WA MOHAMMED DEWJI KWA SIMBA

Mwenyekiti wa Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Moses Katumbi, ameibuka na kumfunda Bilionea mwenzake, Mohamed  Dewji ‘Mo’ ili ajue miiko ya kuwa mwekezaji na 


mshabiki.Dewji licha ya kuwa ndiye mwekezaji Mkuu katika klabu ya Simba, lakini amekuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo kiasi cha kukosa raha pale inapotokea kikosi chake kupoteza mchezo.

Ni juzi katika mashindano ya Mapinduzi CUP wakati timu hiyo ilipopoteza mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kuchapwa bao 1-0, alifikia uamuzi wa kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti wa Bodi lakini baadaye alibatilisha uamuzi wake.

Taarifa imeeleza Katumbi alisema, anatambua machungu ambayo ameyapata  baada ya Simba kufungwa na Mtibwa Sugar katika Kombe la Mapinduzi, lakini ndio mpira ulivyo asitarajie matokeo chanya kila siku.

Alisema, anatambua mchango wake mkubwa ndani ya Klabu hiyo, ambayo kwa sasa inajulikana Afrika nzima, lakini amekuwa akichanganya kazi ya soka pamoja na ushabiki mambo ambayo hayaendi sambamba.

“ Mo anapaswa kupata mafunzo kutoka kwa wawekezaji wakongwe kama sisi, ni mara nyingi timu inaharibu lakini unalia na kufuta machozi kimya kimya, haupaswi kuweka hisia zako kwa mashabiki kwa kuwa wao pia wanakutegemea wewe”

Ushauri wangu kwake, Simba ni Klabu kubwa sana Afrika, asikate tamaa, azidi kupambana, kwani mafanikio ya Simba ni ya taifa la Tanzania sio  mashabiki peke yao,”alisema Katumbi.

Kwa upande wa aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyoo, Crecentius Magori alisema wao kama Simba hawana tatizo lolote na wanashukuru kuona mwekezaji wao Mo amerekebisha kauli ya kujiuzulu na sasa wanaendelea kumtambua kama Mwenyekiti wao.

Hilo limekwisha wanachama watulie, lililotokea jana limefafanuliwa, na ilikua bahati mbaya, kikubwa kwa sasa tuangalie mbele kwa maendeleo ya klabu yetu” alisema Magori.

Aidha Magori amesema wanakabiliwa na kazi kubwa mbele yao hivyo ni vyema wakawa wamoja na kushirikiana kuunga mkono wachezaji wao katika kipindi hiki cha kutetea ubingwa wao.


Post a Comment

0 Comments