BETI NASI UTAJIRIKE

KAPOMBE AZUNGUMZIA HATMA YAKE NDANI YA TAIFA STAZI

Beki bora zaidi wa pembeni upande wa kulia kwa sasa hapa Tanzania Shomari Kapombe amesema bado anahitaji muda wa kujiimarisha kabla ya kufikiria kurudi timu ya Taifa


Kapombe jana aliiongoza Simba mkoani Mwanza kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao Fc katika mchezo uliopgwa uwanja wa CCM Kirumba

Beki huyo mwenye 'mapafu ya mbwa' kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusukuma mashambulizi mbele pamoja na kuzuia, alikuwa bora kwenye mchezo huo
Akizungumza baada ya mchezo, Kapombe alisema ushindi waliopata ni matokeo ya mbinu walizopewa na kocha Sven Vandenbroeck

"Tunamshukuru Mungu kwa kuweza kupata ushindi leo. Haukuwa mchezo rahisi lakini tuliweza kutumia nafasi tulizopata," alisema

Lakini pia waandishi walitaka kufahamu msimamo wake kama ikitokea ameitwa timu ya Taifa kutokana na ubora ambao ameendelea kuonyesha

"Kwa sasa bado siwezi kurudi timu ya Taifa kwani nahitaji kuimarika zaidi. Kikubwa tuendelee kumuomba Mungu labda kwa baadae naweza kurejea"

Kapombe alitangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa mwishoni mwa mwaka jana kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.Mwaka juzi alivunjika mguu wakati akiitumikia Stars nchini Afrika Kusini jeraha ambalo nusura limalize maisha yake ya soka kwani alikaa nje kwa zaidi ya miezi nane

Post a Comment

0 Comments