BETI NASI UTAJIRIKE

BARCELONA YAKALIA KUTI KAVU LA LIGA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Hispania Barcelona wameshindwa kudhihirisha ubora wao baada ya kunga'ang'aniwa sare ya mabao 2-2 na Espanyol. Mchezo huo mkali ulipigwa kwenye dimba la RCDE Stadium linalomilikiwa na Espanyol.

Espanyol walikuwa wakwanza kupata bao dakika ya 23 kupiti kwa David Lopez kabla ya Luis Suarez kuchomoa bao hilo dakika ya 50 na Arturo Vidal kuongeza bao la pili dakika ya 59.

Kadi nyekundu aliyoipata Frenkie Dejong dakika ya 75  ilileta tafurani kwa Barcelona na Espanyol walitumia udhaifu wa eneo la kiungo cha Barcelona kusawazisha bao la pili lililowekwa kimianii na Wu Lei alilofunga dakika ya 88. 

Kwa matokeo hayo Barcelona inaendelea kushika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 40 sawa na mpinzani wake wa jadi Real Madrid mwenye pointi 40.



Post a Comment

0 Comments