BETI NASI UTAJIRIKE

BABA SAMATA AZUNGUMZIA USAJILI WA MBWANA KWENDA ASTON VILLA

Rasmi Mbwana Ally Samata ni mchezaji wa Aston Vila ya Uingereza  na anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza ligi kuu Uingereza maarufu kama English Premier League


Mara baada ya tetesi kusambaa www.amospoti.com ilimtafuta baba mzazi wa mchezaji huyo bwana Ally Samata aliyeonekana kufurahishwa na hatua kubwa anazopiga mtoto wake Mbwana Samata.  Mzee Samata alianza kwa kusema 

"Amenipigia simu saa moja lililopita kwamba yupo safarini kwenda Uingereza kufanyiwa vipimo na baadaye kukamilisha mipango mingine . Nimejikuta natokwa na machozi ya furaha, kubwa namuombea kwa Mungu amfanyie wepesi katika hatua aliyofikia ili atimize ndoto zake za kucheza Ligi kuu Uingereza"

Mara baada ya uhamisho huo kukamilika,Samatta ambaye amefunga mabao 76 tangu ajiunge na miamba ya Ubelgiji Genk akitokea  Tp Mazembe ya Congo anaweka rekodi ya kuwa mtanzania pekee mpaka sasa anayecheza ligi kuu Uingereza.

Habari zisizo rasmi zinasema mchekato wa Samatta kupata vibali  vya kazi umekamilika hivyo anaweza kuanza kuitumikia Aston Villa kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Brighton

Post a Comment

0 Comments