BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA KUWAFUNGA BAO 3 KOCHA WA KAGERA ATUMA SALAMU KWA VIONGOZI WA YANGA

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Meckie Mexime amesema pamoja na kuwa na Leseni A ya ukocha inayotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ambayo inampa sifa ya kuwa



 kocha mkuu wa timu yoyote, yuko tayari kujiunga na Yanga kuwa Kocha Msaidizi
Mexime ambaye juzi aliiongoza Kagera Sugar kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu, amesema anachoangalia ni maslahi na kama Yanga watamlipa zaidi ya anacholipwa na Kagera Sugar atajiunga nao wakati wowote uongozi wa Yanga utamtangaza kocha msaidizi ambaye atashirikiana na kocha mkuu Luc Eymael pamoja na kocha wa viungo Riedoh Berdien ambaye pia ni kocha msaidizi namba mbili

"Nina Leseni A ya Caf (Shirikisho la Soka Afrika), Yanga wananihitaji niwe kocha msaidizi sina tatizo mimi naangalia maslahi wakinipa zaidi ya ninachopata Kagera Sugar nitaenda," alisema kocha huyo.

Hata hivyo Mexime amesisitiza kuwa bado ana mkataba na Kagera Sugar ambao anauheshimu hivyo Yanga inapaswa kumalizana na Kagera Sugar kwanza.Hii si mara ya kwanza kwa kocha huyo kuomba kazi klabuni hapo kwani alishawahi kuomba kazi mwishoni mwa mwaka jana baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo mwinyi Zahera kuondoshwa. 

Post a Comment

0 Comments