Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Difa El Jadida Simon Msuva amewajibu mashabiki wa soka wanaombeza ameshuka kiwango baada ya kusaini na Benfica lakini
hajatambulishwa rasmi na ametupwa kwa mkopo kwenda klabu nyingine inayoshiriki ligi kuu Ureno. Msuva anayecheza Difa El Jadida ya nchini Morocco anategemewa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huku akipigiwa hesabu ya kuanza kuitumikia klabu ya Benfica.
Hapo jana suva alizidi kuonyesha ubora wake kwenye mchezo wa ligi kuu Moroco maarufu kama Botola Pro na walitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Rapide Club na Simon Msuva ndiye aliyefunga bao hilo kwa upande wa timu yake .
Kwa matokeo hayo klabu ya Msuva imeshika nafasi ya 7 ikiwa n pointi 17 ikicheza michezo 11 na anayeongoza msimamo huo ni RSB Berkane aliyecheza michezo 12 na kufikisha pointi 27
0 Comments