BETI NASI UTAJIRIKE

AZAM YALETA MASHINE MPYA LIGI KUU TANZANIA

Viongozi wa Azam FC huwa hawasubiri kesho hasa unapoona mchezaji kijana anafanya vizuri kwenye timu yake na hiilo limeendelea kudhihirika baada ya kunasa sahihi ya Khaleffin Hamdoun aliyekuwa anakipiga mlandege ya Zanzibar Uongozi wa Azam FC, unayofuraha kuwataarifu kuwa tumekamilisha taratibu za kumsajili kiungo mshambuliaji, Khleffin Hamdoun, kwa mkataba wa miaka minne akitokea Mlandege ya Zanzibar.

Huo unakuwa usajili wa kwanza kwa Azam FC kwenye dirisha dogo la usajili, likiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.Hamdoun, aliyefikisha umri wa miaka 19 leo, amesaini mkataba rasmi wa kuitumikia Azam FC leo Jumatano usiku, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'.


Mara baada ya kusaini mkataba huo, kiungo mshambuliaji huyo alielezea furaha yake ya kukamilisha taratibu ya kujiunga Azam FC huku akiahidi kushirikiana na wachezaji wenzake kuipa mataji timu hiyo.

Kiungo mshambuliaji huyo alionyesha kiwango kizuri akiwa na timu yake ya Mlandege ilipochuana na Azam FC juzi, jambo ambalo lilimvutia Cioaba na kuidhinisha asajiliwe haraka iwezekanavyo
.

Post a Comment

0 Comments