BETI NASI UTAJIRIKE

ANTONIO NUGAZ NA HAJI MANARA WATOA NENO KIPIGO CHA YANGA

Klabu ya Yanga hapo jana imepoteza mchezo wake wa pili kwa msimu huu wa 2019/20 baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Kagera Sugar. Matokeo hayo yameishusha Yanga kutoka nafasi ya 4 mpaka nafasi ya 8 huku ikiwa nyuma kwa  pointi 10 


nyuma ya watani zake wa jadi Simba SC.Yanga anapointi 25 huku akicheza michezo 13 huku Simba anapointi 35 akicheza michezo 14 ya ligi kuu  Tanzania bara. Kama kawaida wasemaji wa vilabu hivyo Antonio Nugaz wa Yanga na Haji Manara wa Simba walikuwa na haya ya kusema 

Haji manara aliandika hivi : "Ktk siku mbili hz Washabiki wa Yanga walikuja kwa wingi sana kunitusi hadi kwa wazazi wangu kisa Simba kafungwa.Sikujibu ila nikamwambia Mungu nilipie hili,,kupitia kagera Wamenilipia yale matusi.
Mungu ww ni zaid ya fundi,ww unajiibu kwa ghadhabu kali,niwasihi Wanasimba wenzangu msiwatusi, wafundisheni ustaraab ,Ntarudi baadae kuliko Nyati.

Antonio Nugaz aliandika hivi: "Football Alhamdulilah Mchezo dhidi ya Kagera Sugar tumepoteza kwa goli tatu kwa bila na Mwalimu LUC ameona mapungufu ya kikosi chetu na naamini atayafanyia kazi Insha Allah Shukran kwa mashabiki wetu kwa Kuja Tukutane Jumamosi saa 1 Usiku Uwanja wa Taifa dhidi Azam Fc..

Post a Comment

0 Comments