BETI NASI UTAJIRIKE

ALLY ALLY AFUNGUKA JANJA JANJA ZA VIONGOZI WA YANGA

Baada ya mvutano wa muda mrefu  kati ya Klabu ya Yanga na beki wao Ally Ally hatimae beki huyo amefunguka ishu nzima ya yeye kutaka kutolewa kwa mkopo kwenda klabu ya JKT Tanzania.Stori iko hivi 
Yanga imejikuta na utitili wa mabeki msimu huu huku wote wakiwa mahili kwenye nafasi zao. Ally  Ally ni beki wa kati nafasi ambayo huchezwa na Lamine Moro ,Kelvin Yondani,Dante pamoja na Ally Ally. Uwepo wa mabeki hao umekuwa ni changamoto kwa kocha kuwapanga kwani wote wanaviwango vikubwa hivyo Yanga kwa busara waliamua kumpa nafasi Ally Ally aende kwa mkopo klabu ya JKT Tanzania mpaka mwisho wa msimu ili aweze kupata nafasi ya yeye kucheza .

Ally Ally aelezea ishu nzima 

Dirisha lilikuwa linafungwa usiku halafu siku hiyo hiyo nikaambiwa naenda kwa mkopo JKT Tanzania. . nilikataa nikawaambia nitabaki hapa hapa ntapambana kuhakikisha napigania namba kwa kuwa nina uwezo. . katibu akanijibu SAWA. . Baada ya hapo nikaona taarifa nimetolewa kwa mkopo. . nikawasiliana na katibu akanijibu ni lazima niondoke kwa mkopo. . nikampa masharti nitolewe kwa mkopo kwenda KMC lakini Yanga SC wakakataa. . nilimuuliza katibu sijui hatma yangu kwa kuwa wenzangu walikuwa Singida na mimi nipo njia panda kiukweli sitoweza kuwasiliana naye tena kutokana na majibu aliyonipa ila akanisisitiza siwezi kujiunga na Yanga tena. . kama Yanga hawanitaki ni vema wakavunja mkataba wangu niwe huru kwa maana sasa sielewi hatma"

Post a Comment

0 Comments