BETI NASI UTAJIRIKE

PATRICK AUSSEMS AWAJIBU MASHABIKI WANAOMTAKA AREJEE SIMBA

Aliyekuwa Mkufunzi wa Simba Patrick Aussems amesema amewasikia mashabiki wakishinikiza uongozi umrudishe lakini kwa upande wake hafikirii kurejea nchini Tanzania


Aussems alitimuliwa na Simba mwezi Novemba 2019 baada ya kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuipa ubingwa timu hiyo na kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Kocha huyo ameanza kutajwa na mashabiki wa timu hiyo wakiutaka uongozi kumrejesha kwenye timu baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa, ambapo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo Mo Dewji alitangaza kujiuzulu kabla ya kutangaza kurejea tena.

Aussems amesema kwa upande wake haoni jambo la kushangaza kwa yanayoendelea Simba lakini hakifirii kurejea kutokana na alichofanyiwa awali.

"Siyo jambo zuri kutaka kujua nini wanachokutana nacho Simba kwa sababu kwangu sioni kama kuna kitu kipya ambacho naweza kusema kwa kuwa wanavuna walichopanda wakati naondoka," alisema Aussems
"Unajua katika maisha unapata kile ambacho unastahili kupata na siyo unachotaka kupata sasa na wao wamepata wanachostahili, kifupi siwezi kurejea Simba kwa sababu ilishapita naangalia mambo yangu mengine"

Tangu aondoke Simba Aussems bado hajapata timu ingawa mwenyewe amesema ameamua kupumzika kwa muda kabla ya kurejea tena kwenye majukumu yake

Post a Comment

0 Comments