BETI NASI UTAJIRIKE

ALICHOSEMA KOCHA WA YANGA KUELEKEA MECHI NA AZAM FC

Kocha mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa Kagera Sugar wamewaotea kuwachapa mabao 3-0 hivyo leo watawasha moto mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa.


Eymael alianza kazi yake ya kwanza ndani ya Yanga kwa kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar leo ataongoza jahazi lake kwenye mchezo wa pili dhidi ya Azam FC.


"Tunatarajia upinzani mkali kutoka kwa Azam Fc kwani nimewaona, wana timu nzuri. Sisi tumefanya maandalizi ya kutosha, tunahitaji kushinda mchezo huo," 

"Jioni tumefanya maandalizi ya mwisho, nilipenda tufanye mazoezi usiku kwenye uwanja wa Taifa lakini hatukuruhusiwa. Tutafanya mazoezi mepesi na kuwapa maelekezo ya mwisho wachezaji"

Kocha huyo akazungumzia kipigo walichokutana nacho dhidi ya Kagera Sugar

"Haina maana kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar timu yetu itaendelea kufungwa hapana, walitufunga kwa kuwa walituotea hawataweza kuendelea kutufunga tena tutapambana kufanyia kazi makosa yetu.

"Tatizo bado wachezaji hawajawa na muunganiko mzuri hasa kwenye umaliziaji hapo mambo yakikamilika kila kitu kitakwenda sawa, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.

Yanga imecheza jumla ya mechi 13 ipo nafasi ya nane ikiwa imejikusanyia pointi zake 25 leo itamenyana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 29. 

Post a Comment

0 Comments