BETI NASI UTAJIRIKE

TSHISHIMBI AZUNGUMZIA USAJILI ULIOFANYWA NA YANGA

Achana na matokeo ya mchezo wa jana Jumatano kati ya Yanga na Kagera Sugar, nahodha wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi ameibuka na kuupongeza uongozi wao kwa kufanya usajili matata kwenye dirisha dogo.


Mcongomani huyo anaamini ujio wa nyota wapya waliosajiliwa dirisha dogo, umeongeza uhai na kuziba nafasi zilizoachwa wazi huku akiweka wazi kwamba, nafasi ya kufanya kweli iko wazi na msimu ujao watashiriki michuano ya kimataifa.
Alisema kulikuwa na kina Juma Balinya, Issa Bigirimana, Mayben Kalengo, David Molinga na nyota wengine baada ya kutimuliwa kwao hakuna kinachokumbukwa kutokana na kutua kwa nyota wapya wakali zaidi.

"Usajili uliofanya unahitaji kutoa pongezi kwa viongozi kwani wamefanya kitu ambacho kimerudisha heshima ya klabu wachezaji waliosajiliwa hasa waliopata nafasi ya kucheza kama Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Adeyum Salum na Tariq Seif wameonyesha viongozi hawakukosea kuwasajili," 

Tshishimbi aliiambia www.amospoti.com
"Tunatakiwa kuwapa muda, nategemea watafanya kitu kikubwa zaidi kikubwa ni uongozi kuendelea kuwatengenezea mazingira mazuri ili waendelee kufanya vitu bora zaidi na kuweza kuifanya timu ikiwapa changamoto wapinzani wetu kwenye kila mashindano tutakayoshiriki," alisema.

Tshishimbi aliongeza kwa kuzungumzia suala la kocha mpya Luc Eymael ambapo alifunguka kuwa ujio wake umeongeza changamoto ya wachezaji kupambana lengo likiwa ni kuonyesha nini wanacho ili kujitengenezea mazingira ya kupata namba kikosi cha kwanza.

Post a Comment

0 Comments