BETI NASI UTAJIRIKE

ABDALLAH KING KIBADENI AMTAJA BEKI BORA NDANI YA SIMBA

Kocha wa zamani na mchezaji aliyekipiga Simba Sports Club, Abdallah King Kibadeni, amemchagua Mohammed Hussein kuwa beki wake namba mbili bora dhidi ya Gadiel Michael.


Hivi karibuni kumekuwa na ushindani wa namba baina ya wachezaji hao wawili ndani ya kikosi hicho kiasi cha kwamba imemfanya kocha Sven Vandernbroeck kuwatumia mara kwa mara wote wawili.

Akizungumza na Wasafi FM, Kibadeni ameeleza kuwa kwa namna anavyowaona wachezaji hao wawili anaamini Hussein ndiye anayefiti kuendana na mfumo wanaenda nao Simba.

"Mimi upande wangu Hussein ndiye bora dhidi ya Michael, kwa namna staili ya uchezaji Simba ilivyo naona anafaa kabisa kupewa nafasi ya kwanza.

"Simsemi vibaya Michael, ila kwa mtazamo wangu naamini Hussein ndiye ana uwezo mzuri wa kucheza na nafasi ya beki wa kushoto sababu ni mtulivu"

Post a Comment

0 Comments