BETI NASI UTAJIRIKE

ZIJUE SABABU ZA PELE NA MARADONA KUTOWAHI TWAA TUZO YA BALLON D'OR

Watu wengi wanaweza kujiuliza je Pele na Maradona waliwahi kutwaa tuzo za Ballon D'Or na kama hawakutwaa ni kipi hasa kilipelekea nyota hao hawakustahili kutwaa tuzo hizo


Historia fupi ya Ballon D'or 

Tuzo za Ballon d or zilianzishwa mwaka 1956 na chama cha soka ufaransa na lengo hasa ni kuwatunza wachezaji waliofanya vyema kwa mwaka huo na wenye asili ya Ulaya. Tuzo hizo zilihusiswa na upigwaji kura kwa waandishi wa habari pekee toka mwaka 1956 mpaka 2006 na kuanzia mwaka 2007 makapteni na makocha walipewa nafasi ya kujumuika na waandishi wa habari kwa upigaji kura wa tuzo hizo.

Kutokana na ubora wa tuzo hizo mwaka 2010 shirikisho la soka duniani FIFA liliingia mikataba na Ballon D'or na jina jipya likazaliwa liitwalo FIFA Ballon D Or na mwaka 2016 shirikisho hilo lilijitoa na kuanzisha tuzo zake mpya zifahamikazo kama FIFA WORLD PLAYER OF THE YEAR ambazo Lionel Messi ameshinda kwa mwaka 2019 huku Ronaldo akishinda kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na 2017, Luka Modric alishinda mwaka 2018.


Kulia ni tuzo za Ballon Dor na kushoto ni tuzo za Fifa world best player

Je kipi kilipelekea Maradona na Pele kukosa tuzo za Ballon D'Or 

Pele na Maradona ni wachezaji wa bara la Amerika kusini hivyo tuzo hizo hazikuwahusu kabisa kwa kipindi hicho. Mwaka 1995 Ballon D'or ilianza kutoa tuzo hizo kwa wachezaji wa dunia nzima ndipo mwaka 1995 George Weah alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ulaya kutwaa tuzo hiyo 

Mwaka 1997 Ronaldo De Lima alitwaa tuzo hizo kwa mara ya kwanza akitwaa tena mwaka 2002 huku Rivaldo akitwaa mwaka 1999, Ronaldinho Gaucho akitwaa tuzo hizo mwaka 2005 na Kaka alitwaa tuzo hizo mwaka 2007.




Post a Comment

0 Comments