BETI NASI UTAJIRIKE

ZAHERA AWAKALIA KOONI VIONGOZI WA YANGA

Klabu ya Yanga imejikuta ikiendelea kukalia kuti kavu baada ya aliyekuwa Kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amewataka mabosi wa Yanga kumlipa fedha zake ambazo anadai 


Zahera ambaye ni raia wa Congo, amesema ametoa wiki moja pekee na wasipofanya hivyo ataenda FIFA kushtaki.

Zahera ambaye alifutwa mwezi uiopita  kufuatia kuwa na mwenendo mbaya wa matokeo, ameeleza kutopewa fedha ambazo alikuwa anaikopesha Yanga kutokana na kupitia kipindi kigumu.

Fedha zinajumuisha zile za mishahara ya wachezaji, kulipia nauli ya safari kadhaa za ndege, hela za chakula kwa wachezaji na zinginezo.

Kocha huyo mpaka sasa yupo hapa nchini akiendelea kusubiria fedha hizo ambazo bado anawadai Yanga.

Post a Comment

0 Comments